Kenya yapanga kuzindua mtandao wa 5G mwaka 2022
2022-02-22 08:33:44| CRI

Mkurugenzi wa leseni, viwango na ikibali katika Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CA) Matano Ndaro jana amesema, Kenya itazindua mtandao wa 5G kwa majaribio.

Matano amewaambia waandishi wa habari huko Nairobi kwamba, mamlaka hiyo imetoa mpango unaoeleza mikakati ya kuhimiza maendeleo ya teknolojia ya 5G.

Pia ameongeza kuwa, Kenya itaidhinisha miradi ya kwanza ya majaribio ya 5G na kutoa masafa ya mawimbi yanayohitajika, baadaye itatoa leseni ya biashara ya 5G. Amesema kuwa, makampuni ya mawasiliano ya simu ya Kenya yameanza kupanga miundo mbinu ya 5G kote nchini.