Waziri Mkuu wa Uingereza atangaza kuondoa vikwazo vya COVID-19
2022-02-22 08:42:51| CRI

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametangaza kumalizika kwa vikwazo vyote vya ndani vilivyowekwa kukabiliana na maambukizi ya COVID-19 nchini humo kwa kufuata mchakato utakaoanza baadaye wiki hii.

Waziri mkuu huyo ametangaza kuondolewa kwa sheria hizo katika Bunge la nchi hiyo wakati alipowasilisha mkakati wa serikali wa “kuishi na COVID-19.” Amesema kanuni ya kisheria inayowataka watu wanaogunduliwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona kujitenga itaondolewa kuanzia alhamis wiki hii, na kuongeza kuwa, kuanzia April Mosi, wakati msimu wa baridi utakapomalizika na kupungua kwa kasi ya maambukizi, nchi hiyo itaacha kufanya vipimo vya COVID-19 kwa umma.

Hata hivyo, wasomi, wafanyakazi wa afya na wanasayansi wameeleza wasiwasi wao kuhusu hatua hiyo, wakisema ni mapema sana kupunguza vizuizi wakati bado kuna ripoti nyingi za maambukizi na vifo zinazotolewa kila siku.