Waziri mkuu wa Ethiopia asema uchumi wa nchi hiyo unaendelea vizuri licha ya changamoto mbalimbali
2022-02-23 08:05:56| CRI

Waziri mkuu wa Ethiopia asema uchumi wa nchi hiyo unaendelea vizuri licha ya changamoto mbalimbali_fororder_VCG111283324799

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema jana kuwa, nchi hiyo imeweza kudumisha ukuaji wa uchumi licha ya changamoto mbalimbali, ikiwemo mapigano katika sehemu ya kaskazini mwa nchi hiyo.

Akijibu maswali yaliyoulizwa na wabunge wa nchi hiyo kuhusu maendeleo ya uchumi wa nchi hiyo katika nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha ulioanza Julai 8, 2021, Waziri Mkuu huyo amesema nchi hiyo imekusanya asilimia 14.9 zaidi ya mapato kuliko kipindi kama hicho katika mwaka wa fedha uliopita.

Amesema mageuzi ya kiuchumi yaliyotoka ndani ya nchi hiyo yamesaidia kutuliza biashara ya nje ya nchi hiyo na hivyo kupunguza ukosefu wa usawa kati ya usafirishaji na uingizaji wa bidhaa.