Idadi ya watu waliofariki katika mlipuko wa mgodi nchini Burkina Faso yafikia 63
2022-02-23 08:05:23| CRI

Idadi ya watu waliofariki katika mlipuko uliotokea jumatatu wiki hii katika mgodi wa dhahabu kusini magharibi mwa Burkina Faso imeongezeka na kufikia 63.

Gavana wa mkoa wa Kusini-Magharibi, Emmanuel Zongo amesema, mgodi huo umefungwa mpaka itakapotangazwa tena.

Chanzo cha mlipuko huo bado hakijafahamika, na uchunguzi unaendelea.