Mawaziri wa mambo ya nje wakutana DRC kwa maandalizi ya mkutano wa kanda ya Maziwa Makuu
2022-02-23 08:06:24| CRI

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zilizosaini makubaliano ya Mfumo wa Amani, Usalama na Ushirikiano (PSCF) kwa Jamhuri ya Kidemokraisa ya Congo (DRC) na kanda ya Maziwa Makuu barani Afrika wamekutana jana jumanne katika mji mkuu wa nchi hiyo Kinshasa, ikiwa ni maandalizi ya mkutano wa ngazi ya juu kuhusu utekelezaji wa makubaliano hayo.

Mkutano huo ulioongozwa na Waziri wa Maingiliano ya Kikanda na Nchi Zinazoongea lugha ya Kifaransa wa DRC, Didier Mazenga, ni maandalizi ya mkutano wa ngazi ya juu wa Utaratibu wa Kikanda wa Utaratibu wa Usimamizi wa makubaliano ya PSCF unaotarajiwa kufanyika hii leo.

Katika mkutano huo, wakuu wa nchi za Kanda ya Maziwa Makuu watafanya tathmini ya maendeleo na changamoto zilizopo katika utekelezaji wa makubaliano hayo.