Katibu Mkuu wa UM alaani kukamatwa kwa walinzi wa usalama nchini CAR
2022-02-24 08:30:38| CRI

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana amelaani vikali kukamatwa kwa askari 4 wa Tume ya Kulinda Amani ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA) na kutaka askari hao waachiwe huru mara moja.

Askari hao walikamatwa jumatatu na polisi wa CAR huko Bangui wakati wakimsindikiza ofisa mmoja mwandamizi wa tume hiyo.

Bw. Guterres amesisitiza kuwa, kwa mujibu wa makubaliano kati ya Umoja huo na serikali ya CAR kuhusu hadhi ya MINUSCA hiyo mwaka 2014, askari wa tume hiyo wana haki na kinga zinazoendana na maslahi ya Umoja wa Mataifa. Pia ameongeza kuwa, makubaliano hayo yameweka mchakato halisi ikiwa askari wa tume hiyo kushukiwa kuwa mhalifu na serikali ya CAR, lakini kesi hiyo haikufuata mchakato huo.