Watu 11 wafariki katika mlipuko wa ugonjwa wa surua kusini mwa DRC
2022-02-24 08:23:21| cri

Kaimu Mkuu wa jimbo la Lomami la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) amesema, watu 121 wameambukizwa ugonjwa wa Surua na 11 kati yao wamefariki tangu mlipuko wa ugonjwa huo ulipotokea Januari 8 mwaka huu katika jimbo la Lomami kusini mwa nchi hiyo.

Surua ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi ambao huathiri zaidi watoto. Kwa sasa hakuna tiba ya surua, na njia bora zaidi ya kuzuia ugonjwa huo ni kupata chanjo.