WFP yasema ukame unaoendelea unaathiri Pembe ya Afrika
2022-02-24 08:32:01| CRI

WFP yasema ukame unaoendelea unaathiri Pembe ya Afrika_fororder_VCG31N143079097

Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) limesema ukame unaoendelea katika eneo la Pembe ya Afrika unaongeza athari zinazotokana na changamoto mbalimbali katika eneo hilo.

Shirika hilo limesema, watu karibu milioni 13 wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na ukosefu wa maji kutokana na ukame katika eneo la mashariki mwa Pembe ya Afrika.

Kwa mujibu wa Shirika hilo, ukame unaathiri maeneo ya Pembe ya Afrika ambayo katika mwaka uliopita yaliathiriwa na mapigano, mafuriko ya ghafla, bei kubwa ya chakula, uvamizi wa nzige wa jangwani, na athari za kiuchumi na kijamii kutokana na janga la COVID-19.