Mtaalam wa Ghana asema ushirikiano wa China na Afrika katika sekta ya miundombinu utaboresha biashara ya ndani
2022-02-24 08:31:11| CRI

Mchumi kutoka Ghana, Abena Oduro, amesema ushirikiano kati ya Afrika na China katika sekta ya miundombinu utaboresha maingiliano ya biashara ya ndani katika bara hilo.

Akizungumza na Shirika la Habari la China Xinhua, Oduro amesema maendeleo ya miundombinu ya biashara yatakuwa muhimu katika mafanikio ya utekelezaji wa Eneo la Biashara Huria la Afrika (AfCFTA).

Amesema, Afrika inaweza kutumia vizuri wenzi wake wa kimataifa ikiwemo China kwa ajili ya maendeleo ya ujenzi wa njia za reli na miundombinu mingine ya usafirishaji pamoja na maendeleo ya kiviwanda kwa ajili ya ushirikiano wa kunufaishana.

Ameongeza kuwa, Pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja lililotolewa na China linaweza kusaidia maingiliano yatakayorahisisha biashara ya ndani ya Afrika, na kwamba bara hilo linahitaji njia za reli na mtandao muhimu wa barabara unaounganisha maeneo muhimu ya Afrika.