UNECA kuzindua kituo cha kwanza cha utafiti wa AI barani Afrika
2022-02-24 08:31:36| CRI

Kamati ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (UNECA) imetangaza kuwa iko tayari kuzindua Kituo cha kwanza cha Utafiti wa Akili Bandia (AI) barani Afrika katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kongo, Brazzaville.

Kituo hicho kitakachozinduliwa baadaye wiki hii na UNECA pamoja na serikali ya Jamhuri ya Kongo, ni kituo muhimu kitakachojizatiti zaidi katika kuendeleza utafiti kupitia akili bandia ili kuendeleza teknolojia ya kidijitali barani Afrika katika maeneo ya sera za kidijitali, miundombini, fedha, ujuzi, majukwaa ya kidijitali na ujasiriamali.