Nchi za Afrika Mashariki kufanya luteka ya pamoja ya kijeshi nchini Uganda
2022-02-24 10:26:19| cri

 

 

Jeshi la Uganda jana limesema, zaidi ya askari 1,500 kutoka nchi 6 wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) vitafanya luteka ya ya pamoja ya kijeshi nchini humo.

Taarifa iliyotolewa na jeshi la Uganda imesema, askari kutoka Uganda, Tanzania, Kenya, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini wataungana na raia katika Luteka hiyo ya 12.

Luteka hiyo itafanyika mwezi Mei na Juni kwenye Mashriki mwa Uganda, ambayo itajaribu utayari wa vikosi vya usalama katika kukaibliana na changamoto ngumu za usalama.