Kenya yaunganisha umeme kwa kaya milioni 8.6
2022-02-25 08:45:30| CRI

Kenya imeunganisha umeme kwenye kaya karibu milioni 8.6 mpaka kufikia mwezi Desemba mwaka jana, ikiwa ni ongezeko kutoka milioni 7.3 mwezi Januari mwaka 2020.

Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Nishati na Mafuta (EPRA) nchini humo Daniel Kiptoo amewaambia wanahabari kuwa, Kenya ni nchi pekee ya Afrika Mashariki ambayo asilimia 75 ya wananchi wake wanapata huduma ya umeme.

Amesema ongezeko la upatikanaji wa umeme ni hatua kubwa katika kutimiza ruwaza ya maendeleo ya nchi hiyo ya mwaka 2030, ambayo inataka kuibadili Kenya kuwa nchi mpya ya kiviwanda na kipato cha kati itakapofika mwaka 2030.