Afrika yaelekea lengo la kutoa chanjo kwa asilimia 70 ya idadi ya watu
2022-02-25 10:10:34| cri

 

 

Shirika la Afya Duniani (WHO) jana limesema, kiwango cha utoaji wa chanjo barani Afrika bado ni cha chini zaidi duniani, na bara hilo linaelekea kutimiza lengo la kutoa chanjo kwa asilimia 70 ya idadi ya watu.

Katika taarifa yake, Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika Dr. Matshidiso Moeti, amesema, karibu dozi milioni 400 zimetolewa barani Afrika katika mwaka mmoja uliopita tangu mpango wa Covax ulipotoa awamu ya kwanza ya dozi za chanjo ya COVID-19 kwa Afrika mwaka jana,

Hata hivyo, amesema ni asilimia 13 tu ya waafrika wamepata chanjo kamili ya COVID-19, na ni nchi 18 tu ambazo zimetimiza viwango vya kutoa chanjo kwa asilimia chini ya asilimia 10 , na nchi 3 zimetimiza asilimia chini ya 1.