Russia yatoa sharti la kufanya mazungumzo na Ukraine
2022-02-25 08:43:34| CRI

Russia yatoa sharti la kufanya mazungumzo na Ukraine_fororder_VCG111370650223

Katibu wa mawasiliano ya ikulu nchini Russia, Dmitry Peskov jana amesema, Russia iko tayari kufanya mazungumzo na Ukraine kama nchi hiyo itakuwa tayari kufanya mazungumzo kuhusu hadhi yake isiyopendelea upande wowote na kutoweka silaha nchini.

Peskov amesema lengo la Russia la kufanya operesheni maalumu dhidi ya Ukraine ni kuifanya Ukraine isiwe na silaha, ili kuhakikisha usalama wa Russia.

Habari nyingine zinasema, makao makuu ya jeshi la Ukraine yametoa taarifa ikisema, hadi kufikia jana saa saba mchana kwa saa za huko, jeshi la Russia lilifanya mashambulizi zaidi 30 dhidi ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Boryspil mjini Kiev na maeneo mengine yaliyolengwa, na kukanusha madai kuwa jeshi la Russia limefika Odessa.