ECOWAS kuongeza kasi ya Bima ya Afya kwa Wote itakapofika mwaka 2030
2022-02-25 08:45:03| CRI

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) kupitia Shirika la Afya la Afrika Magharibi (WAHO) linatafuta kuongeza kasi ya upatikanaji wa Bima ya Afya kwa Wote (UHV) kwa nchi wanachama itakapofika mwaka 2030.

Mkurugenzi Mkuu wa WAHO, Stanley Okolo amesema hayo katika ufunguzi wa mkutano wa kilele wa Usimamizi wa Afya ya Wote wa ECOWAS na Mkutano maalum wa Mawaziri wa Afya wa ECOWAS uliofanyika mjini Accra, Ghana. Amesema lengo jipya la afya la kikanda, limeundwa kwa kuzingatia mambo matatu muhimu, ambayo ni kuongeza kasi ya upatikanaji wa huduma za afya ambazo ni jumuishi na nafuu, kuhakikisha maandalizi mazuri na ya ufanisi kwa afya ya umma na uwezo wa kujibu majanga katika kanda hiyo, na kuimarisha michakato ya WAHO na kuboresha ufanisi wake katika uongozi.