Shirika la Kupambana na Dawa za Kulevya la Nigeria lakamata wauza dawa za kulevya 7
2022-02-28 14:06:07| CRI

Shirika la kupambana na dawa za kulevya nchini Nigeria limesema limemkamata kiongozi mkuu mwanamke wa dawa za kulevya na watuhumiwa wengine sita, pamoja na kupata kilo 5,862 za dawa za kulevya zikiwemo codeine huko Lagos.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, Shirika la Kitaifa la Kutekeleza Sheria ya Dawa za Kulevya limesema maafisa wa kupambana na dawa za kulevya walivamia Jumamosi saa 3 asubuhi kwenye ngome ya dawa za kulevya iliyopo katika mtaa wa Gambari na kumkamata mkuu wao na wengine sita. Msemaji wa shirika hilo, Femi Babafemi amesema wahalifu hao walishambulia maafisa kwa mawe, chupa na bunduki, wakizuia wakuu wengine wasikamatwe pamoja na kuwakomboa watuhumiwa waliokamatwa pamoja na vithibiti vya dawa za kulevya.

Shirika limewaonya wale wote wanaotumiwa na magenge ya dawa za kulevya kuwazuia au kuwashambulia maafisa wa kupambana na dawa za kulevya wasifanye kazi zao, kuacha ama watakabiliwa na adhabu kali.