Kenya kuboresha miundombinu ya kikanda ili kustawisha biashara kati ya nchi za Afrika
2022-03-01 10:37:19| CRI

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya aahidi kuboresha miundombinu kwenye kanda hiyo ili kustawisha biashara kati ya nchi za Afrika.

Rais Kenyatta amesema kwenye hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Bw. James Macharia, Waziri wa Uchukuzi, Miundombinu, Nyumba, Maendeleo ya Miji na Kazi ya Umma, kuwa serikali ya Kenya itaendelea kujenga mtandao wa barabara ili kuunganisha ushoroba wa uchukuzi wa kaskazini unaounganisha nchi zisizo na bandari katika Afrika Mashariki na bandari ya Kenya Mombasa.

Bw. Macharia amesema kuwa hawawezi kunufaika kikamilifu na Eneo la Biashara Huru la Afrika (AfCFTA) bila ya miundombinu iliyoendelezwa vizuri.

Pia amesisitiza kuwa Kenya itaweka kipaumbele katika Maendeleo ya mradi wa LAPSSET ambao utatoa njia mbadala ya usafirishaji wa mizigo na abiria kati ya Kenya na nchi jirani za kaskazini.