Waandamanaji wa Sudan wadai utawala wa kiraia mbele ya Ikulu
2022-03-01 10:35:28| CRI

Waandamanaji wa Sudan wadai utawala wa kiraia mbele ya Ikulu_fororder_3

Maelfu ya waandamanaji nchini Sudan Jumatatu walivunja uzio wa kiusalama na kufika kwenye milango ya ikulu ya Sudan wakidai utawala wa kiraia.

Mashuhuda wamesema maandamano hayo makubwa yalifanyika jana Jumatatu katika mji mkuu, Khartoum na miji mingine, ambapo waandamanaji wanadai utawala wa kiraia na kuzitaka mamlaka kuwaadhibu waandamanaji wanaodaiwa kuwa wauaji. Vikosi vya polisi vilivyotumia mabomu ya machozi dhidi ya waandamanaji vimelazimishwa kurudi kwenye vituo vyao, huku askari jeshi wakijipanga mbele ya milango ya ikulu ya Sudan na kwenye sehemu za kuingilia karibu na barabara bila ya kuwaingilia waandamanaji.

Waandamanaji walitoa sauti zao wakisema “madaraka ni kwa ajili ya watu, na jeshi ni kwa ajili ya kambi”, wakilitaka jeshi kukabidhi madaraka kwa serikali ya kiraia.