Tume Mpya nchini Somalia kujikita kwenye mchakato wa kuleta utulivu na ujenzi wa nchi
2022-03-02 09:45:04| CRI

Tume Mpya ya Kulinda Amani ya Umoja wa Afrika nchini Somalia ambayo itaitwa Tume ya Mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) itajikita kwenye mchakato wa kuleta utulivu na ujenzi wa nchi ikiwa na lengo wazi mbele yake.

Hayo yamesemwa jana na Kamishna wa Masuala ya Kisiasa, Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika, Bankole Adeoye, kwenye taarifa iliyotolewa Mogadishu nchini Somalia, akiwa kwenye ziara ya siku tatu nchini humo, ambapo amekutana na maafisa wa ngazi ya juu wa serikali, wadau wa asasi za kiraia na washirika wa kimataifa wa Somalia. Kamishna Adeoye amesema ATMIS inaungana kwa asilimia 100 na Mpango wa Mpito wa Somalia, ikimaanisha kuwa mkakati wa serikali ya Somalia na madhumuni ya ATMIS vitafungamana, na hii ndio sababu moja kubwa inayoleta tofauti.

Kamishna Adeoye amesema safari hii ATMIS itakuwa na kikosi chepesi ambacho kitaweza kupunguza, kuangamiza na kuharibu makundi yenye silaha ambayo yanafanya maisha ya watu wema wa Somalia yawe magumu.