Makubaliano ya kusitisha vita nchini Sudan Kusini yazidi kuwa kwenye hatari ya kuondolewa
2022-03-03 10:02:21| CRI

Makubaliano ya usitishwaji vita nchini Sudan Kusini yanazidi kuwa kwenye hatari ya kuondolewa kufuatia mapigano makali ya hivi karibuni katika majimbo ya Upper Nile na Unity.

Asrat Denero Amad, mwenyekiti mpya wa Utaratibu wa Mpito wa Kusimamisha Vita (CTSAMVM), chombo ambacho kinasimamia Makubaliano ya usitishaji uhasama ya mwaka 2017, ameonya kwamba kuna hatari ya kuondolewa makubaliano hayo kutokana na vurugu zinazotokea kila mara. Amesema kuhusu masuala muhimu ya usitishwaji vita wa kudumu, kuna wasiwasi kwamba makubaliano hayo yamekumbwa na shinikizo na yanaweza kuvunjika, pia kuna maeneo ambayo hivi sasa ni wazi yanadhoofishwa.

Januari mapigano yalizuka katika jimbo la Upper Nile, kati ya kundi la SPLA-IO lililo chini ya makamu wa kwanza wa rais Riek Machar na wanajeshi wanaoongozwa na Ochan Puot ambaye alijiondoa kwa waasi hao mwishoni mwa mwaka jana na kujiunga na jeshi la sudan kusini (SSPDF).