Vyombo vya habari vya Kenya vyasema nchi za Afrika zitafuatilia Mikutano Miwili ya China
2022-03-03 10:03:49| CRI

Vyombo vya habari vya Kenya vyasema nchi za Afrika zitafuatilia Mikutano Miwili ya China_fororder_3

Hivi karibuni China itaingia katika kipindi cha “Mikutano Miwili”. Makala iliyotolewa kwenye Tovuti ya Shirika la Utangazaji la Kenya KBC imeeleza kuwa, Mikutano Miwili ikiwa ni mikutano muhimu sana ya China ambayo ni kundi la pili la kiuchumi duniani, itafuatiliwa sana na jamii ya kimataifa.

Makala hiyo imeeleza kuwa, mikutano hiyo itahitimisha matokeo ya kazi ya serikali ya China katika mwaka uliopita, na kuweka malengo ya maendeleo kwa mwaka unaofuata. Kama ilivyokuwa mwaka uliopita, mkutano wa mwaka huu vilevile utafanyika wakati wa mapambano dhidi ya COVID-19, ndiyo maana juhudi za China za kuzuia kwa mafanikio maambukizi ya virusi hivyo na kudumisha utulivu wake wa kiuchumi pia zitafuatiliwa katika mikutano hiyo.

Pia imesema kuwa, ufunguaji mlango wa China, pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” pamoja na ushirikiano na mazungumzo na nchi nyingine ni maudhui mengine muhimu. China ikiwa mshirika mkubwa wa kibiashara wa Afrika, uwekezaji wake barani Afrika umekuwa ukiongezeka katika miaka miwili iliyopita. Afrika imefaidika na uwekezaji wa China haswa katika sekta ya ujenzi na afya. Hayo yanatokana na kuwa viongozi wa Afrika wanapenda kujenga uhusiano mzuri na China ili kujiendeleza, hali ambayo imedhihirisha kuwa jaribio la kutengeneza nadharia ya “Diplomasia ya Mtego wa Madeni” ili kuvunja ushirikiano kati ya Afrika na China halitafanya kazi.