Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani nchini Tanzania yatishiwa na shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu
2022-03-03 10:00:42| CRI

Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani nchini Tanzania yatishiwa na shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu_fororder_4

Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani, iliyoanzishwa mwaka 1997 na mamlaka za Tanzania ili kuhifadhi mimea na wanyama wa Milima ya Usambara Mashariki, inatishiwa na shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu.

Fikiri Maiba, mhifadhi mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) amesema zaidi ya ekari 20 za misitu ya asili zimeharibiwa na wachimbaji madini katika miaka ya hivi karibuni. Maiba amewaambia waandishi wa mazingira waliotembelea eneo hilo linalolindwa, kwamba Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani ni chanzo cha maji kwa watu zaidi ya 200,000 wanaoishi mkoa wa Tanga. Amesema vijana wanajihusisha zaidi katika shughuli za uchimbaji madini kwenye hifadhi hiyo, na kuongeza kuwa TFS imeunda kikosi kazi kitakachofanya doria mara kwa mara ili kulinda hifadhi hiyo.

Kwa mujibu wa afisa huyo wachimbaji wadogo wamevamia misitu, na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira kwa kuangusha miti mikongwe ya asili yenye thamani ili kuchimba dhahabu.