Sierra Leone yaanzisha mradi wa kujifunza Kichina katika shule za msingi
2022-03-04 10:32:07| CRI

Sierra Leone imeanzisha mradi wa kujifunza misamiati ya Kichina katika shule tano za msingi kwa lengo la kuhimiza lugha ya Kichina nchini humo.

Mradi huo unaojulikana kama “Small-Small Chinese” ulianzishwa na Mariatu Kargbo, mwanamke wa Sierra Leone aliyefanya kazi kama msanii nchini China. Kwenye hafla ya uzinduzi Bi. Karbo alisema mradi huo utawezesha wanafunzi wa shule za msingi kuwasiliana kwa Kichina rahisi na kuwanufaisha baadaye wakati watakapojiunga rasmi kwenye taasisi za Confucius au shule nyingine. Naibu Waziri wa Elimu ya Msingi na Sekondari Emily Gogra amepongeza hatua hiyo na kushauri kwamba iingizwe kwenye mtaala wa shule.

Kwa upande wake balozi wa China nchini Sierra Leone Hu Zhangliang ameelezea mradi huo kama njia muhimu ya kufunza Kichina kwa shule tano za msingi. Amemshukuru mwanzilishi kwa juhudi zake kubwa za kuhimiza urafiki na maelewano kati ya China na Sierra Leone.