Kenya kuanzisha utaratibu wa kupambana na biashara haramu ya viumbepori
2022-03-04 10:31:31| CRI

Kenya imezindua utaratibu kwenye taasisi za fedha ili kukabiliana na biashara haramu ya viumbepori.

Waziri wa Utalii na Wanyamapori, Najib Balala amesema mjini Nairobi kuwa utaratibu huo unakusudia kusaidia taasisi za fedha kutambua, kukabiliana na kuripoti miamala inayotia shaka ambayo inahusiana na biashara haramu ya viumbepori.

Utaratibu huo unajumuisha jukwaa ambalo litaiwezesha Kenya kuimarisha na kutoa taarifa za uhalifu wa viumbepori ambazo zitapelekea kukamatwa na kuzuia biashara ya viumbepori. Amebainisha kuwa Kenya imedhamiria kupambana na biashara haramu ya viumbepori hususan kuokoa spishi zilizo hatarini, na kusisitiza kuwa utekelezaji kamili wa utaratibu huo utachangia kulinda wanyama na mimea kwa faida ya vizazi vijavyo.