Wanaharakati wahimiza uwekezaji unaozingatia binadamu ili kuharakisha mabadiliko ya kijani
2022-03-07 09:15:56| CRI

Wanaharakati wamesema, mabadiliko ya kijani yenye haki, ustahimilivu barani Afrika yatatimizwa kama serikali na wakopeshaji watatoa rasilimali nyingi zaidi katika mapendekezo yanayolenga kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Wanaharakati wa kijani huko Nairobi wametoa taarifa ikisema, ukuaji wenye kiwango cha chini cha utoaji wa hewa za kaboni barani Afrika, unahitaji kutoa kipaumbele kwa jamii wakati wa kutoa fedha kupunguza madhara na kuzoea mabadiliko ya tabianchi.

Mtaalamu wa sera za tabianchi wa Kenya Bw. Robert Muthami, amesema wakati nchi za Afrika zinainua nia zao za kufikia uwiano wa kaboni, zinatakiwa kuzingatia mahitaji ya jamii za msingi zinazoathiriwa zaidi na maafa ya asili.