Tanzania yauza tani zaidi 5,000 za nyama kwa nchi za nje ndani ya miezi saba
2022-03-08 09:07:20| CRI

Waziri wa mifugo na uvuvi wa Tanzania Bw. Mashimba Ndaki, amesema Tanzania imeuza tani 5,362.9 za nyama zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 22.4 kwa nchi za nje kati ya mwezi Julai mwaka 2021 na mwezi Januari mwaka 2022, ambalo ni ongezeko la asilimia 200.

Amesema mafanikio makubwa ya mauzo ya nyama nchi za nje yanatokana na kuboreshwa kwa sera na mikakati katika sekta ya nyama iliyotolewa na serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan. Nyama hiyo iliuzwa kwa Comoro, Saudi Arabia, Vietnam, Qatar, China, Bahrain, Kuwait na Oman.