Nchi za Afrika zatoa wito wa kuimarisha kwa pamoja sera za kuhimiza maendeleo endelevu
2022-03-08 08:54:11| CRI

Nchi za Afrika zimesisitiza haja ya kuimarisha kwa pamoja sera za kuhimiza maendeleo endelevu na ufufukaji baada ya janga la Corona, ili kuhakikisha zinaondokana na athari za janga hilo.

Wito huu umetolewa baada ya Jukwaa la Nane la Kikanda kuhusu Maendeleo Endelevu (ARFSD-8) kuridhia Azimio la Kigali kuhusu utendaji mzuri na ufumbuzi wa kuimarisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu barani Afrika.  

Azimio la Kigali linatoa wito kwa nchi za Afrika kutumia nyenzo mpya, masuluhisho ya kivumbuzi na teknolojia, ikiwemo kupitia ushirikiano ulioimarishwa na sekta binafsi, akademia, mashirika yasiyo ya kiserikali, asasi za kiraia na wadau wengine, katika kujenga mifumo imara ya takwimu ya kitaifa iliyo nyumbufu, endelevu na shirikishi.