Kenya yafikiria kuanzisha mfuko wa chai ili kudumisha utulivu wa bei
2022-03-08 09:17:09| cri

Wizara ya kilimo ya Kenya imesema mfuko maalumu wa chai utaanzishwa ili kuhamasisha raslimali kwa ajili ya kudumisha utulivu wa bei kwa ufanisi zaidi.

Waziri wa kilimo, mifugo, uvuvi na ushirika nchini Kenya Peter Munya, amesema mfuko huo utatumika kupunguza athari za hali tete ya soko kwa wakulima wa chai, kuwafidia wakulima wadogo wa chai na kuunga mkono ujenzi wa maghala katika viwanda. Mfuko huo utatunishwa kwa kipindi cha miaka miwili kwanza, kabla ya kuruhusu kukopa.

Bw. Peter Munya ameongeza kuwa wafanyabiashara wanaojiunga na mfuko huo (CUF) watafurahia sera za upendeleo zikiwemo msamaha wa ushuru wa kuingiza bidhaa na kodi ya ongezeko la thamani. Pia kwa kuokoa gharama ya nguvukazi, serikali itashirikiana na tasnia husika kuendeleza maelezo juu ya matumizi ya mitambo ya kuvuna chai.