EAC: Wanawake ni muhimu kwa mafanikio ya kiuchumi ya Afrika Mashariki
2022-03-09 08:41:52| CRI

Taarifa iliyotolewa Jumatatu na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inasema, wanawake wanachukua zaidi ya asilimia 50 ya watu wote katika jumuiya hiyo, kwa hiyo wao ni ufunguo wa mafanikio ya kiuchumi ya kanda hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa mjini Arusha, kaskazini mwa Tanzania, katibu mkuu wa EAC Bw. Peter Mathuki amesema wanawake wanapaswa kushirikishwa katika utoaji wa maamuzi kwenye ngazi za kitaifa na kikanda, kwa lengo la kuhakikisha maamuzi yanakuwa shirikishi na kuakisi mahitaji ya watu wote.