Kenya na UM kushirikiana kuunda jukwaa la pamoja la kuzuia vurugu katika uchaguzi
2022-03-09 09:36:09| cri

Kenya na Umoja wa Mataifa wameanzisha jukwaa la amani Jumanne wiki hii ili kuzuia vurugu wakati wa uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika tarehe 9 Agosti.

Mwakilishi mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Kenya Bw. Walid Badawi amesema umoja huo utatoa msaada wa kifedha na kiufundi kuzuia migogoro na kuitikia hali ya dharura. Ameeleza kuwa jukwaa hilo litatoa mfumo wa tahadhari na kushughulikia mizozano inayoweza kutokea wakati wa uchaguzi, na kutambua maeneo yanayoweza kukumbwa na tatizo hilo.

Mwenyekiti wa Tume ya Mshikamano na Utangamano wa Kitaifa ya Kenya (NCIC) Bw. Samuel Kobia, amesema jukwaa hilo lilianzishwa katika msingi wa kukadiria changamoto za usalama na amani zinazoweza kutokea katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka huu.