UM: Ukame wasababisha watu 845,000 kupoteza makazi nchini Ethiopia na Somalia
2022-03-09 09:23:09| CRI

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema ukame nchini Ethiopia na Somalia umesababisha watu 845,000 kupoteza makazi na mifugo zaidi ya milioni 1.5 kufa nchini Ethiopia pekee.

Bw. Dujarric amesema Umoja wa Mataifa na washirika wake wameongeza misaada kwa watu walioathiriwa na ukame na kutoa chakula kwa watu zaidi milioni 2.7 nchini Ethiopia, na watoa misaada ya kibinadamu wanasambaza chakula kwa watoto wenye utapiamlo.

Aidha ameongeza kuwa fedha za ziada zinahitajika kwa haraka kwa kuwa mahitaji yanatarajiwa kuongezeka zaidi. Mpango wa msaada wa kibinadamu kwa Somalia unatafuta dola za kimarekani bilioni 1.5 kwa ajili ya kuwasaidia wasomali milioni 5.5 walio hatarini zaidi, na mpaka sasa ni asilimia 3.3 tu ya fedha hizo zimepatikana.