Tanzania yatoa lita laki moja za dawa ya kupambana na viwavijeshi
2022-03-10 08:59:43| CRI

Wizara ya kilimo ya Tanzania imetangaza kutoa lita laki moja za dawa ya kupambana na viwavijeshi waliovamia chakula na mashamba ya mazao ya biashara katika wilaya 39 nchini Tanzania.

Waziri wa kilimo wa Tanzania Bw. Hussein Bashe amesema dawa hiyo inatolewa kwa wakulima bila malipo kwa lengo la kuwahimiza kuwaangamiza wadudu hao. Bw. Bashe ametangaza kutolewa kwa dawa hiyo baada ya ukaguzi wa hekta elfu 70 za mahindi zilizovamiwa na viwavijeshi katika wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma. Amewataka wakurugenzi watendaji na maofisa wa kilimo kwenye wilaya zote 39 zilizovamiwa na viwavijeshi kuwapatia wakulima dawa hizo.

Mwishoni mwa mwezi uliopita vyombo vya habari viliripoti kuharibiwa kwa hekta elfu 12 za chakula na mazao ya biashara mkoani Lindi kusini mwa Tanzania.