Tanzania yapongeza matumizi ya teknolojia ya kilimo cha uyoga ya China kuhimiza kilimo endelevu
2022-03-10 09:00:37| CRI

Serikali ya Tanzania imepongeza matumizi ya teknolojia ya “Juncao” ya kupanda uyoga kwenye mboji kuhimiza kilimo endelevu na ufugaji nchini Tanzania.

Waziri wa mifugo na uvuvi wa Tanzania Bw. Mashimba Ndaki, amesema serikali ya Tanzania imetoa maombi ya fedha kutoka kwa serikali ya China kwa ajili ya utekelezaji wa teknolojia hiyo kwa ajili ya chakula cha wanyama na uzalishaji wa uyoga.

Teknolojia hiyo ina manufaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na uzalishaji wa uyoga, utengenezaji wa dawa, kupambana na mmomonyoko wa udongo na kulinda ardhi yenye rutuba, na kuhimiza maendeleo ya ufugaji.

Bw. Ndani pia amesema teknolojia hiyo itasaidia kuongeza upatikanaji wa malisho na kuongeza tija kwenye ufugaji, itakayopunguza umaskini na kuongeza pato la taifa.