Uganda yashika nafasi ya tano katika Farahisi ya Masoko ya Fedha ya Afrika ya Absa mwaka 2021
2022-03-10 09:22:50| CRI

Uganda imeshika nafasi ya tano kwa kupata alama 57 kati ya nchi 23 zilizoorodheshwa kwenye Farahisi ya Masoko ya Fedha ya Afrika ya Absa mwaka 2021.

Uchunguzi wa Absa uliotolewa huko Kampala umeonesha kuwa Uganda imepanda kutoka nafasi ya 10 ikilinganishwa na uchunguzi uliofanywa mwaka 2020.

Uchunguzi huo umetathmini maendeleo ya soko la fedha katika nchi 23 na kuonyesha chumi zenye mazingira yanayounga mkono masoko yenye ufanisi.
Uchunguzi huo umeonesha kuwa Ghana na Uganda zimeingia kwa mara ya kwanza katika nafasi tano za mwanzo, huku nchi zote mbili zikipata alama za maendeleo. Afrika Kusini, Mauritius na Nigeria zimedumisha nafasi zao za uongozi katika farahisi hiyo, ingawa alama zilizozipata nchi hizo tatu mwaka jana zilishuka.

Katika kanda ya Afrika Mashariki, Uganda imeshika nafasi ya kwanza ikifuatwa na Kenya iliyopata alama 47, huku Tanzania ikipata nafasi ya tatu kwa alama 45 na kufuatwa na Rwanda kwa alama 43 na Ethiopia iliyopata alama 25.