Mawaziri wa China, Ufaransa na Italia wabadilishana maoni kuhusu suala la Ukraine
2022-03-11 09:58:07| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana kwa nyakati tofauti alibadilishana maoni na wenzake wa Ufaransa na Italia kwa njia ya video kuhusu hali ya Ukraine.

Bw. Wang alipowasiliana na waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Bw. Jean-Yves Le Drian alisema mwafaka mkuu uliofikiwa kati ya viongozi wa China, Ufaransa na Ujerumani katika mkutano wa video uliofanyika Jumanne unapaswa kutekelezwa ipasavyo. Kwenye mkutano huo Rais Xi Jinping wa China alisisitiza umuhimu wa kuheshimu mamlaka na ukamilifu wa ardhi wa nchi zote, kufuata kikamilifu Katiba ya Umoja wa Mataifa,kutilia maanani ufuatiliaji wote halali wa nchi zote kuhusu masuala ya usalama, na kuunga mkono juhudi zote zinazosaidia utatuzi wa mgogoro wa sasa kwa njia ya amani.

Bw. Wang amesisitiza kuwa msimamo wa China ni thabiti na ni wazi, na inapenda kuona mapigano yanasitishwa mapema ambayo pia ni matarajio ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa.