Msomi wa Kenya: Mikutano Miwili ya China yaakisi dhana ya maendeleo inayotoa kipaumbele kwa maslahi ya umma
2022-03-11 10:00:23| CRI

Msomi wa Kenya: Mikutano Miwili ya China yaakisi dhana ya maendeleo inayotoa kipaumbele kwa maslahi ya umma_fororder_1541616304

Msomi wa Kenya Bw. Adhere Cavince hivi karibuni alipohojiwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG amesema, Mikutano Miwili ambayo ni Mkutano wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China na Mkutano wa Bunge la Umma la China, ni mbinu ya kivumbuzi ya China katika utawala wa nchi. Mikutano hiyo inayofanyika kila mwaka inatoa jukwaa kwa viongozi wa China na wajumbe kutoka sekta mbalimbali na vyama vya kidemokrasia kuwasiliana ana kwa ana, na kufanya majumuisho ya matarajio ya umma kwenye usanifu wa ngazi ya juu wa maendeleo ya nchi. Anaona Mikutano hii Miwili inaakisi dhana ya maendeleo ya China inayotoa kipaumbele kwa umma, na inasaidia kuimarisha mshikamano wa wananchi chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC).

Bw. Cavince amesema, China imetimiza lengo la maendeleo la Miaka 100 ya Kwanza, na kuanza safari mpya ya kuijenga China kuwa nchi ya kisasa ya kijamaa na kuelekea lengo la Miaka 100 ya Pili. Mikutano Miwili inayofanyika katika hali ya sasa, ina umuhimu mkubwa hasa kufuatia China kuongoza duniani katika maendeleo ya uchumi na mapambano dhidi ya janga la COVID-19 katika mwaka 2021. Amesema dunia nzima inafuatilia maamuzi yatakayotolewa kwenye Mikutano Miwili ya China kutokana na hadhi muhimu ya China kwenye kufufua na kutuliza uchumi wa dunia.Bw. Cavince amesema anafuatilia zaidi hatua zitakazotolewa kwenye Mikutano Miwili katika kuhimiza ustawi wa pamoja. Anaona ikiwa ni tofauti na nchi nyingi duniani, China imeshughulikia vizuri uhusiano kati ya serikali na soko, na kutoruhusu mitaji iwe juu ya sheria. Anaona kutoa kipaumbele kwa maslahi ya umma katika utungaji wa sera, kunasaidia kuhamasisha nguvu na hamasa ya umma, na hivyo kuwezesha kutimizwa kwa malengo mbalimbali ya maendeleo ya uchumi na jamii.