Jumuiya ya Afrika Mashariki yazitaka nchi wanachama kuimarisha mwitikio wa kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza
2022-03-11 08:56:04| CRI

Jumuiya ya Afrika Mashariki imezitaka nchi wanachama kuimarisha hatua za kuzuia na kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza kufuatia mvua kubwa zinazonyesha katika baadhi ya maeneo ya jumuiya ya Afrika Mashariki.

Taarifa iliyotolewa na jumuiya hiyo imesema mwito huo umetolewa kufuatia mlipuko wa homa ya manjano nchini Kenya uliosababisha vifo vya watu watatu, na taarifa ya sektretarieti ya jumuiya hiyo kuhusu uwepo wa homa ya bonde la ufa miongoni mwa mifugo katika jumuiya hiyo.

Ofisa mwandamizi wa jumuiya hiyo Bw. Christophe Bazivamo, amezitaka nchi wanachama kuripoti milipuko hiyo kwa shirika la afya duniani WHO na shirika la kimataifa la afya ya wanyama OIE. Pia amezitaka nchi zote wanachama kuanzisha vituo vya ufuatiliaji, udhibiti na kutoa chanjo ya homa ya manjano.