UA na UM watoa wito pande za Sudan kurejesha mazungumzo
2022-03-11 10:11:06| CRI

Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa umeonya dhidi ya matokeo ya mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini Sudan na kutoa wito kwa pande mbalimbali za kisiasa kurejesha haraka mazungumzo.

Balozi maalumu wa Umoja wa Afrika nchini Sudan Bw. Mohamed Hacen Lebatt na kiongozi wa Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan UNITAMS Bw. Volker Perthes, wamefanya mkutano wa pamoja na wanahabari huko Khartoum ukiwa ni sehemu ya juhudi za pamoja za mashirika hayo kuhimiza mazungumzo kati ya pande za Sudan.

Bw. Lebatt amesema viashiria vyote vilivyopo sasa kwa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa vinaonesha kuwa Sudan iko katika hali ya hatari kubwa, na kama watu wakishindwa kukubaliana, kutakuwa na matokeo yasiyotakiwa.

Bw. Perthes amesema makubaliano yoyote kuhusu utaratibu wa kipindi cha mpito na taasisi za utawala, hasa kuhusu uteuzi wa waziri mkuu, lazima yawe ya watu wa Sudan.