Huawei kutoa masuluhisho ya kisasa ya kuhifadhi Data ili kuendeleza taasisi za kifedha nchini Kenya
2022-03-11 08:59:38| CRI

Kampuni ya Tehama ya China Huawei imesema itatoa masuluhisho ya kisasa ya kuhifadhi Data kwa ajili ya kuhimiza maendeleo ya taasisi za kifedha nchini Kenya.

Andy Luo, mkurugenzi wa masuluhisho wa Huawei kanda ya Afrika Mashariki, ameliambia kongamano moja la teknolojia mjini Nairobi kuwa, kampuni hiyo imezindua mfumo wake mpya wa kuhifadhi Data wa Ocean Protect, uliosanifiwa kufaa vituo vya Data vyenye ukubwa tofauti.

Akiongea kwenye Kongamano la Huawei Africa Tour, Bw. Luo amesema kutokana na kuongezeka kwa huduma za kifedha, thamani ya miamala inaongezeka kwa kasi, hali inayohitaji mifumo ya kisasa ya kuweza kutuma data kubwa kwa ufanisi, hasa sekta ya benki siku zote inahitaji miundombinu yenye uhakika na inayotegemeka ili kuepuka hasara kubwa za kiuchumi zinazoweza kuletwa na upotevu wa data na kukatika kwa huduma.