Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Walemavu ya Beijing yafungwa
2022-03-14 08:09:04| CRI

Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Walemavu ya Beijing yafungwa_fororder_VCG31N1384823028

Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Walemavu ya Beijing imefungwa jana usiku katika Uwanja wa michezo wa Taifa mjini Beijing katika hafla iliyohudhuriwa na rais Xi Jinping wa China na rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki ya Walemavu, Andrew Parsons.

Katika siku 9 zilizopita, wanamichezo karibu 600 kutoka nchi na sehemu 46 wameshindana kwenye uwanja wa michezo na kuonyesha moyo wa kujitegemea na kujiendeleza.

Bw. Parsons amepongeza michezo hiyo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Walemavu ya Beijing ambayo amesema imefanyika kwa usalama, uaminifu na kwa ubora, na kuweka kiwango kwa Michezo mingine ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Walemavu.