Msomi wa Nigeria: Mafanikio ya Michezo ya Olimpiki ya Majira Baridi ya Beijing ni ushindi wa China, na pia ni ushindi wa dunia
2022-03-14 09:08:36| CRI

Msomi wa Nigeria: Mafanikio ya Michezo ya Olimpiki ya Majira Baridi ya Beijing ni ushindi wa China, na pia ni ushindi wa dunia_fororder_558285969

Machi 13, Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing ilifungwa kwa mafanikio, na kutimiza ahadi ya China ya kuandaa “Michezo Miwili yenye Ubora Sawa (Two Games of Equal Splendor)”. Msomi wa Nigeria Bw. Adekunle Osidipe alipohojiwa hivi karibuni na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG), alisema, mafanikio ya michezo hiyo miwili ya Olimpiki ni ushindi wa China, na pia ni ushindi wa dunia.

Bw. Adekunle Osidipe anaona kuwa, wakati dunia inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kuendelea kuibuka kwa mawimbi mapya ya maambukizi ya COVID-19 na kupamba moto kwa migogoro ya kikanda, China imeshikilia kuandaa Michezo ya Olimpiki ya Majira Baridi ya Beijing na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira Baridi ya Beijing kama ilivyopangwa, na kufanikisha tamasha kubwa la michezo duniani ambalo ni alama ya mshikamano na urafiki. Amesema, “Mji wa Michezo Miwili ya Olimpiki” utatoa urithi muhimu wa matumaini na imani kwa dunia nzima.

Bw. Adekunle Osidipe amesema, michezo hiyo miwili ya Beijing inawafanya watu waamini kuwa, licha ya sintofahamu zilizosababishwa na janga la Corona na migogoro ya kikanda, dunia bado inaweza kujumuika pamoja kwenye viwanja vya michezo na kushindana kwa uhuru kwenye mazingira ya kirafiki. Amesema, katika dunia yetu inayohitaji mshikamano, mafanikio ya michezo hiyo miwili ya Olimpiki ya majira baridi ya Beijing yameamsha matumaini ya watu wa nchi mbalimbali, na kuimarisha imani yao katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili.