Watu 75 wafariki katika ajali ya treni nchini DRC
2022-03-14 08:23:15| CRI

Watu 75 wamefariki na wengine 175 kujeruhiwa alhamis iliyopita baada ya treni kutoka kwenye njia yake katika wilaya ya Lubudi, mkoa wa Lualaba, kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokraisa ya Kongo (DRC).

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli nchini humo Fabien Mutombo amesema, treni hiyo ilitoka kwenye njia na kusababisha mabehewa kadhaa kuanguka kwenye bonde.

Ajali za treni zinazoteka mara kwa mara katika sehemu hiyo kutokana na hali mbaya ya treni na njia za reli zilizoharibika.