Watu 10 wauawa katika shambulizi kwenye mgodi wa dhahabu nchini Burkina Faso
2022-03-14 08:24:18| CRI

Watu karibu 20 wasiojulikana waliokuwa na silaha walishambulia mgodi wa dhahabu ulioko Baliata katika mkoa wa Sahel, nchini Burkina Faso jumamosi iliyopita na kusababisha vifo vya watu 10 na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Ripoti zinasema, alhamis iliyopita, watu 14 waliuawa katika shambulizi kwenye mgodi mwingine wa dhahabu ulioko mkoa wa Seytenga.

Hali ya usalama nchini Burkina Faso imekuwa mbaya zaidi tangu mwaka 2014, huku mashambulizi ya kigaidi yakisababisha vifo vya watu zaidi ya 1,000 na wengine zaidi ya milioni moja kukimbia makazi yao.