Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaongeza msaada wa kukabiliana na ukame nchini Somalia
2022-03-15 08:31:27| CRI

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaongeza msaada wa kibinadamu ili kupunguza athari mbaya iliyotokana na ukame nchini Somalia.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulika na Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (UNOCHA) jana imesema, hali ya dharura ya ukame nchini Somalia imeongezeka, huku idadi ya watu walioathiriwa ikiongezeka hadi takriban watu milioni 4.5, kutoka milioni 3.2 mwezi Desemba 2021, na idadi hii inazidi kuongezeka.