Kimbunga Gombe chasababisha vifo vya watu 15 nchini Msumbiji
2022-03-15 08:58:06| CRI

Kimbunga Gombe chasababisha vifo vya watu 15 nchini Msumbiji_fororder_VCG111373235747

Kimbunga cha kitropiki cha “Gombe” kimesababisha vifo vya watu 15 na kuathiri zaidi ya watu 98,000 nchini Msumbiji.

Habari zilizotolewa na Redio ya Taifa ya Msumbiji zinasema, kimbunga hicho kilisababisha mvua kubwa na mafuriko, na kati ya watu waliofariki, wengi walikufa kwa kuangukiwa na nyumba au miti. Takwimu za awali zinaonesha kuwa zaidi ya watu 98,000 wameathiriwa, na kati yao watu 12,000 wamepata msaada.

Kulingana na shirika la habari la serikali ya Msumbiji, kimbunga cha “Gombe” kilitua kwenye pwani ya jimbo la Nampula nchini humo asubuhi ya tarehe 11, na sasa kinaelekea kusini mwa Malawi.