Mwanahabari mwandamizi wa Jamhuri ya Kongo: Maamuzi yaliyotolewa kwenye Mikutano Miwili ya China yataiathiri dunia nzima
2022-03-15 12:18:06| CRI

Mwanahabari mwandamizi wa Jamhuri wa Kongo: Maamuzi yaliyotolewa kwenye Mikutano Miwili ya China yataiathiri dunia nzima_fororder_1193022464

Mikutano Miwili ya China iliyomalizika hivi karibuni, ambayo ni Mkutano wa tano wa Baraza la 13 la Mashauriano ya Kisiasa la China na Mkutano wa tano wa Bunge la 13 la Umma la China, imefuatiliwa na jumuiya ya kimataifa. Mwanahabari mwandamizi kutoka Jamhuri ya Kongo Bw. Brinel Liwata alipohojiwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, amesema kuwa wakati dunia inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kuendelea kuibuka kwa mawimbi mapya ya maambukizi ya virusi vya Corona na kupamba moto kwa migogoro ya kikanda, maamuzi yaliyotolewa kwenye Mikutano Miwili ya China kuhusu maendeleo ya China katika siku zijazo si kama tu yanaiathiri China, bali pia yataiathiri dunia nzima.  

Bw. Liwata anaona kuwa, katika hali ya sasa yenye changamoto nyingi, China imeweka lengo lake la ukuaji wa uchumi kwa mwaka huu kuwa asilimia 5.5, kiwango ambacho anaona kinafaa na ni cha mantiki. Amesema, wakati uchumi wa dunia unafufuka polepole, dunia nzima hasa Afrika imeitupia macho China, kwa kuwa uchumi wa China unachukua nafasi muhimu katika mchakato wa ufufukaji wa uchumi wa dunia, na matokeo ya ushirikiano na China yana umuhimu mkubwa kwa karibu nchi zote za Afrika. Akitolea mfano wa Jamhuri ya Kongo, amesema ushirikiano kati yake na China umeboresha kwa kiasi kikubwa miundombinu yake, na makao makuu mapya ya Bunge yaliyojengwa kwa ufadhili wa China ni matokeo mapya ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Bw. Liwata amesema, kupitia Mikutano Miwili ameona fursa za China na vilevile uzoefu wa China. Mikutano Miwili ni mpango muhimu wa kimfumo unaojumuisha matarajio ya wananchi kwenye usanifu wa ngazi ya juu wa maendeleo ya taifa. Kwenye Mikutano Miwili ya mwaka huu ulinzi wa haki halali za wanawake na watoto ulikuwa moja ya mada kuu, hali ambayo inaakisi mwitikio wa serikali kuu kwa matarajio na ufuatiliaji wa umma, ambao utaimarisha zaidi mshikamano katika jamii ya China.

Bw. Liwata amesema, “Sera zote zilizotungwa na serikali ya China zinalenga kuzidisha maslahi ya umma, na Chama cha Kikomunisti cha China na serikali ya China wameweka mfano wa kuigwa katika nyanja hii.”