Iran haitavumilia uwepo wa “vituo vya njama” karibu na mipaka yake
2022-03-15 08:51:14| CRI

Iran haitavumilia uwepo wa “vituo vya njama” karibu na mipaka yake_fororder_伊朗外交部发言人Saeed Khatibzadeh

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Saeed Khatibzadeh amesema, nchi hiyo haitavumilia uwepo wa “vituo vya njama” karibu na mipaka yake.

Khatibzadeh alitoa kauli hiyo jana katika mkutano na wanahabari, kufuatia kujibu shambulizi la makombora lililofanywa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislam ya Iran (IRGC) katika kituo cha ujasusi cha Israel kilichopo katika mji mkuu wa mkoa wa Kurdish, Erbil.

Amesema haikubaliki kuwa moja ya nchi jirani, ambayo ina uhusiano na maingiliano ya kina na Iran, inaweza kuwa kituo cha matishio dhidi ya nchi hiyo, na kuongeza kuwa, mara kadhaa Iran imeitaka serikali ya Iraq kutoruhusu makundi yanapingana na Iran kutumia ardhi yake kwa vitendo kama hivyo.

Vituo viwili vya ujasusi vya Israel vililengwa katika shambulizi la makombora mapema jumapili, ambapo kundi la IRGC lilisema shambulizi hilo ni majibu ya shambulizi la anga lililofanywa na Israel katika mji mkuu wa Syria, Damascuc wiki iliyopita, ambapo maofisa wawili wa kundi hilo waliuawa.