Mkoa wa Pwani nchini Tanzania wazindua operesheni ya kupambana na wahamiaji haramu
2022-03-15 08:29:23| CRI

Mamlaka ya mkoa wa Pwani nchini Tanzania jana umezindua operesheni kubwa ya siku 10 inayolenga kuwakamata wahamiaji haramu wanaotafuta hifadhi mkoani humo.

Mkoa huo unatumiwa na magenge ya kusafirisha binadamu kama mlango wa kusafirisha wahamiaji haramu, hasa wanaotokea Pembe ya Afrika.

Mkuu wa mkoa huo Aboubakar Kunenge alipotangaza operesheni hiyo inayoanza tarehe 14 hadi 23 mwezi huu, amesema lengo la operesheni hiyo ni kuchunguza, kuthibitisha na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu wote wanaoishi katika eneo hilo kiharamu.