China yajutia hatua ya Marekani ya kulazimisha lugha ya haki za binadamu katika azimio la Baraza la Usalama kuhusu Sudan Kusini
2022-03-16 08:45:06| CRI

Naibu Balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Dai Bing amejutia lugha ya lazima iliyotumiwa na Marekani katika muswada wa azimio la haki za binadamu la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kuongezewa muda wa Kikosi cha Ulinzi wa Amani cha Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS).

Balozi Dai amesema, China ililazimika kususia kura iliyopigwa jumanne baada ya Marekani, ambaye ni mwandishi wa azimio hilo kuhusu Sudan Kusini, kukataa kufanya marekebisho.

Balozi huyo amesema, UNMISS kimefanya juhusi kubwa na endelevu katika kuwezesha utekelezaji wa Makubaliano ya Ufufukaji, ulinzi wa raia, kusambaza misaada ya kibinadamu, na kusaidia ujenzi wa taifa la Sudan Kusini. Akizungumza sababu za kususia kupiga kura baada ya kura hiyo, Balozi Dai amesema China inapongeza nafasi muhimu ya Kikosi hicho na kuunga mkono kuongezewa muda wa majukumu yake.

Hata hivyo, Balozi Dai amesema, katika mchakato wote wa majadiliano, Marekani ililazimisha kujumuishwa kwa maneno mengi yanayohusiana na haki za binadamu, na matokeo yake ni muswada ambao hauna uwiano.