Somalia yatoa wito wa msaada wa haraka kutokana na ukame mkali nchini humo
2022-03-16 08:36:40| cri

Somalia yatoa wito wa msaada wa haraka kutokana na ukame mkali nchini humo_fororder_f31fbe096b63f6244807c8e2031537f11b4ca350

Serikali ya Somalia imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuipatia misaada ya kibinadamu, ikisema watu milioni 6.9 wameathiriwa na ukame mkali unayokumba maeneo mengi nchini humo.

Katika taarifa yake iliyotolewa jumatatu mjini Mogadishu, Waziri Mkuu wa nchi hiyo Bw. Mohamed Roble amesema, ukame umeathiri karibu watu milioni 6.9 na zaidi ya mifugo milioni 9.5, huku watu milioni 2.6 wakikabiliwa na uhaba mkubwa wa maji. Pia amewataka wafadhili kuharakisha kutoa misaada kwani hali ya ukame inazidi kuwa mbaya.